Wekeza Faida Kukuza Mtaji - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Wednesday 3 January 2018

Wekeza Faida Kukuza Mtaji



Habarini za leo waungwana
Baada ya sikukuu na tumeanza mwaka siku zinayoyoma ada zinasubiria kodi za nyumba na mahitaji mbalimbali ya kijamii 
Kwa wake ambao ni wajasiriamali na wengine wameishafika kwenye uchumi wa kati katika biashara zetu kuna haja ya kujua namna ya kutumia faida kukuza mtaji.
Faida ni mtaji unaopatikana kutoka kwenye mtaji halisi baada ya kutoa matumizi katika mapato baada ya kipindi maalumu ulichojiwekea katika uzalishaji wako hiyo haiangalii umetumia nyongeza nje ya mtaji wakati unapotaka kupata faida chukua mtaji halisi toa matumizi katika kuendesha biashara yako kinachobakia ndio faida.
Kwanini kuna haja ya kuwekeza faida 
1. Hasara isiyoonekana
Wengiwetu tumekua hatuchanganui hasara katika biashara pale inapotokea hasara isiyoonekana faida ndio itatumika kuziba pengo la mtaji wako 
2. Kukua kwa biashara
Katika biashara yeyote ile ambayo inausimamizi mzuri inakua na kuongezeka badala ya kukimbilia kwenye taasisi za fedha kuomba mkopo faida iliyowekezwa kwa malengo inaweza kutumika pale mtaji wa nyongeza unapohitajika 
3. Changamoto za biashara
Katika biashara kukosekana kwa changamoto ni jambo lisiloepukika kwani kuna kipindi wateja wanakuwa hawapo na upatikanaji wa malighafi unakuwa ni wachangamoto, kupanda na kushuka kwa bidhaa sokoni na changamoto mbalimbali as kiuchumi ambazo haziepukiki katika biashara yeyote. Hivyo faida inayopatikana inafaa kutumika vyema katika kuziba changamoto zilizopo katika 

Kuwekeza faida kunatokana na mahitaji yaliyopo kwenye biashara yako( kwakuanzisha biashara nyingine yeye kutoa faida haraka na isiyochukua muda mrefu kuona faida m.f uuzaji wa vyinywaji laini, ice cream, maji n.k) au kuwekeza kwenye taasisi za fedha kwa kutumia akaunti za malengo, fixed asset na kuwekeza katika soko la hisa au katika saccos au vicoba kwa namna ambayo ni rahisi kwako, kuna haja ya kuwekeza faida yako kwenye dhamana rafiki endapo ukiihitaji unaweza kuichukua bila kuwa na changamoto zozote.
Kwanini tuwekeze faida watu wengi hususani wafanyabiashara wadogo wamejikuta wakifanya matumizi kwa kutumia faida pale ambapo biashara inayumba kunakuwa 1. Kuomba mkopo 2. Kufunga biashara hali inakuwa tofauti kama umewekeza faida yako ni wakati muafaka wa kuitumia.
Uwekezaji upo wa aina mbalimbali hivyo ni vyema ufanye maamuzi sahihi ya kuwekeza faida ili iwe mtaji wako wa baadae 
Ni matamanio na matumaini yangu kuona tunanufaika na makala hii fupi ambayo inaweza kutujenga wote kwa pamoja katika kuhakikisha tunafanikiwa na kufikia malengo yetu katika biashara zetu
Ahsante sana

Ndimi 

SIA EDWARD.

No comments:

Post a Comment