Biashara nzuri ni ipi? - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Monday 11 December 2017

Biashara nzuri ni ipi?



Karibu tena mpenzi msomaji wa blog ya jikitenafursa.blogspot. com siku tutaenda kuzungumzia ni biashara gani nzuri Mara nyingi biashara limekuwa daraja linawavusha wengi kwenda kwenye mafanikio na uhuru wa kipato .

Biashara ni nini?
Biashara ni kitendo ya kuuza na kununua kwa malengo yakupata Faida,  hiyo ndiyo huitwa biashara yaani unayoifanya kukupatia Faida.

Zipi sifa za biashara nzuri?

Biashara nzuri ama yeny ubora Mara nyingi wataalamu husema ni ile biashara inayogusa maisha ya wanajamii kwa maana ni ile inayolenga kutatua kero Fulani kwenye jamii ambayo kwa kipindi Fulani jambo hilo lilikuwa changamoto kwa jamii husika na wewe ukaja ukaweka utatuzi wa tatizo hilo , biashara hiyo itakuwa bora na nzuri 
Zifuatazo ni sehemu ya sifa za biashara bora...

a). Biashara yenye kukujenga kiakili.
Tafuta biashara itayo kujenga kiakili , biashara ya aina hii ni ile ambayo haikufanyi kuwa mtumwa wa biashara  bali ni biashara itakayokupa fursa ya kuwekeza kichwa pia kwa maana ya kwamba biashara hiyo itakufanya uwe na maarifa na weledi kichwani kwako kwa mfano unatoa huduma ya chakula kwa jamii chakula hicho unachohudumia kwenye siku hadi siku utakuwa mtu bora zaidi kwenye mapishi na kuhudumia.

b). Biashara yenye kutoa kipato bakia.

Biashara nzuri ni ile itakayo kupatia kipato cha kubakia yaani (residual income) ubakiaji wa kipato hicho kitaanza kukusukuma kuelekea kwenye mafanikio makubwa na kukupatia Uhuru wa kipato kwa kipindi hats cha miaka mitatu.

c)Biashara inayokufanya kila siku uwe mbunifu.

Mara nyingi biashara nzuri huwafanya wamiliki wake kuwa wabunivu kila Mara kwa kuangalia mapungufu yaliyopo kwenye huduma , bidhaaa, eneo , na hata bei ya bidhaa kwa kiasi kikubwa biashara itayokuwa na ubunivu wa kila Mara huwavuta watu mara dufu kwani kile wanachokitafuta wanakipata bila kukosa.

d).Biashara yenye kuanza na mtaji Mdogo.

Biashara nzuri ni ile yenye kuanza kidogo kidogo na baadaye kukua na kuwa kubwa zaidi hii inamfanya mmiliki wake kuwa na uwezo wa kujua na kutambua fursa na changamoto Zinazoweza kujitokeza kwa biashara yake na kuchukua tahadhari kwakua amekuwa nayo biashara hiyo toka utotoni Mwa biashara hiyo.

e). Biashara inayotumia sayansi na Tekinolojia
Ni bayana sasa kuwa mabadiliko ndilo jambo lenye nguvu sana duniani Leo ulimwengu umehama toka mifumo ya kawaida na kwenda mifumo ya juu ya ufanyaji mambo , hususani hata biashara Leo biashara nyingi zinaendeshwa kwa mawasilino jifunze kuchukua mawasiliano ya wateja wapigie kuwajulia hali waeleze ingizo la bidhaa mpya , Tangaza biashara yako watu wapate kuifahamu maana huwezi kutaka kukua na ukaacha mambo yanakufanya ukue kibiashara navyo ni pamoja na ukuaji wa teknolojia 
Jitahidi Biashara yako ipo kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, what's app, Instagram n.k

Makala hata yameandikwa na Michael Charles 0759880010. 


 


No comments:

Post a Comment