Fursa Ya Kiafya Kwa Kitunguu Swaumu - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Sunday 10 December 2017

Fursa Ya Kiafya Kwa Kitunguu Swaumu

KITUNGUU SAUMU

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaaluma, huitwa allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.

HAYA NI BAADHI YA MAGONJWA YALIYOTHIBITIKA KUTIBIKA AU KUKINGWA NA KITUNGUU SWAUMU:

1. Huondoa sumu mwilini
2. Husafisha tumbo
3. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
4. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
5. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
6. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
7. Huondoa Gesi tumboni
8. Hutibu msokoto wa tumbo
9. Hutibu Typhoid
10. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
11. Hutibu mafua na malaria
12. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
14. Hutibu upele
15. Huvunjavunja mawe katika figo
16. Hutibu mba kichwani
17. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
18. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
19. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
20. Hutibu maumivu ya kichwa
21. Hutibu kizunguzungu
22. Hutibu shinikizo la juu la damu
23. Huzuia saratani/kansa
24. Hutibu maumivu ya jongo/gout
25. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
26. Huongeza hamu ya kula
27. Huzuia damu kuganda
28. Husaidia kutibu kisukari
29. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
30. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu

            ANGALIZO

Mama mjamzito chini ya miezi 4, asitumie kitunguu saumu, chaweza sababisha madhara.


1 comment:

  1. Asante sana kwa hili, kwa kweli vitunguu saumu ni muhimu kutumia kila siku kwenye vyakula.

    ReplyDelete