Unyanyapaa na Umaskini - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Wednesday 3 January 2018

Unyanyapaa na Umaskini



Leo tutazame kidogo unyanyapaa katika hali ya kawaida tumesikia unyanyapaa ukitajwa  kwenye nyanja ya afya kwa upana wake kuwa ni kutengwa na jamii na watu wanaokuzunguka kutokana na ugonjwa unaoambukiza kwa njia mbalimbali zinazotambulika kitabibu.
Hali hiyo imepelekea muhusika kupata msongo wa mawazo na kumpelekea kujiona hana thamani katika maisha yake.
Katika maisha yetu ya kila siku tumekumbana na unyanyapaa wa kiuchumi kifikra na kimawazo ambao kwenye afya madhara ya unyanyapaa ni kifo ila kwenye maisha ni umasikini. 
Katika tafiti mbalimbali za kiuchumi zimetoa tafsiri mbalimbali ya umasikini kwa muonekano wake lakini kiuhalisia ni hali ya kushindwa kujikimu mahitaji muhimu kama chakula, malazi, afya, elimu na mavazi n.k 
Wale wote ambao wanaitwa masikini leo hii na kwenye tafiti mbalimbali wametokana na unyanyapaa wa kifikra na mawazo. Tutaendelea kuwa na matabaka haya hadi pale kila mmoja watu ataona kuna haja ya kuishi bila unyanyapaa. Wale ambao tunawaita masikini wamejikuta kwenye fursa lakini wamekosa kushirikishi kimamilifu katika fursa chanya na hata wakishirikishwa wamekuwa wakikutana na vikwazo kama:- 

1. Kutengwa 
2. Elimu
3. Miundombinu 
4. Magonjwa
5. Taarifa hafifu 
6. Msongo wa mawazo
7. Kutojikubali 
8. Mawasiliano 
9. Fikra hafifu 
10. Unyanyapaa wa mtu mwenyewe 

Tutaendela kuwa na matabaka ya kiuchumi kama vikwazo hivyo kumi (10) havitatendewa kazi na kutengenezewa mifumo thabiti ya kumsaidia muhusika 
Katika awamu ya tatu (3) na nne (4) kulikuwa na programu ya MKUKUTA na MKURABITA na TASAF ambayo ipo mpaka leo lakini kwanini tumeendelea kuona matabaka ya watu wa hali duni na walioko kwenye umaskini uliokithiri ukishamiri na kukua.
Ni ukweli usiopingika tumepata neema katika awamu ya nne (4) lakini leo watu watasema and "vyuma vimekaza" hii ni matakwa ya mtu binafsi kuwa na unyanyapaa wa ndani na msongo wa mawazo ambaye anawaza kupata kidogo kushibisha tumbo lake. 
Kumekuwepo na makundi mbalimbali ya wwakinamama na mabinti wameanzisha VICOBA lakini vingi vinaishia hewani kuna haja ya kutengeneza mifumo stahiki na kutoa elimu sahihi kuwafanya watu hawa kujitenga na unyanyapaa waweze kujikwamua na umasikini 
Hali ya unyanyapaa ndani ya vikundi hivi imeendelea kushamiri na kukua kwa kasi bila kuwepo kwa tabibu na mtoa nasaha ambaye anaweza kuvisaidia ili viweze kujikwamua
Tutaendelea na makala hii kwenye nyanja ya elimu kipindi kijacho 
Hivyo basi tutengeneze mazingira ya kuondokana na umasikini kwa kupiga vita unyanyapaa kwa kila mpenda maendeleo 
Ahsante sana  




No comments:

Post a Comment