A to Z ya Kuanzisha Biashara ya Vipodozi. - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Friday 5 January 2018

A to Z ya Kuanzisha Biashara ya Vipodozi.


Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa makala katila blog yako pendwa ya jikite na fursa ....

Mwaka sasa umeanza kusonga bila mkwamo wa aina yoyote na huenda ungependa Mwaka huu kuanzisha biashara na ya wewe kukuingizia kipato ni vyema sasa pia ukawaza pia kuhusu biashara hii ya Vipodozi maana waswahili husema akipendacho binti/mwanamkea hakikosi kununiliwa , pia vipodozi ni moja ya hitaji muhimu sana kwa wanawake.

NIFANYE NINI SASA NIKITAKA KUANZISHA BIASHARA HII..?,

Kwanza inabidi upate eneo zuri na lenye nafasi ya kutosha kuweka vipodozi na kufanya biashara hii , Jengo liwe na mwanga wa kutosha na liruhusu mzunguko mzuri wa hewa.

Pili inabidi uwe na namba ya mlipa kodi (TIN) kutoka TRA kwa ajili ya kulipia kodi biashara yako na kupata leseni 

Tatu unapaswa uende kwenye mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) hapo utaonana na maafisa husika na leseni za biashara ya vipodozi kwa ajili ya ukaguzi wa eneo unalotaka kufanyia biashara ya vipodozi na watakutoza ada ya ukaguzi. 
Wakimaliza kukagua na kukubaliana na eneo basi watakutaka ulipie kibali na leseni ili uweze kuruhusiwa kuanza biashara hii. 

MAMBO MENGINE MUHIMU NI YAPI?
Kuna mambo ya Msingi kabisa kabla ya kuyatimiza ya ya juu niliyoyataja nayo ni..

1.MTAJI.
Hakuna kiasi maalum ambacho unatakiwa kuanza nacho , cha Msingi ni wewe mwenyewe unajiwezaje , duka lako liwe na ukubwa gani ama hadhi gani na kuwa linapaswa kuwa na vitu gani?

Gharama kubwa huwa zipo kwenye kodi ya jengo la biashara , shelf , na makabati ya aluminium na vipodozi vya bei kubwa kama vile perfume original
Pamoja na hayo mtaji wa kuanzia unaweza kuanzia milioni tano kwa duka kubwa , ni muhimu pia kuwa na malengo makubwa kwa kuanza kidogo kidogo

2. CHANGAMOTO ZA BIASHARA HII.
kama unavyofahamu hakuna biashara isiyo kuwa na changamoto ni muhimu kufahamu unapingia kwenye biashara kuwa inazo changamoto zake pia . 
Biashara hii inachangamoto hizi 
a) mahitaji ya wateja
b) vipodozi feki 
c) kuna ukaguzi wa Mara kwa Mara 

Karibu sana ndimi Michael Charles.


5 comments:

  1. Jaman dadang anashid na kazi ya duka la vipondozi naomba nisaidieni yupo Dar naomba msaada wenu Namba yangu hii 0656486453🙏🙏🙏🙏🙏🙏

    ReplyDelete
  2. Jaman dadang anashid na kazi ya duka la vipondozi naomba nisaidieni yupo Dar naomba msaada wenu Namba yangu hii 0656486453🙏🙏🙏🙏🙏🙏

    ReplyDelete
  3. Ahsanten sana kwa kutuelimisha

    ReplyDelete
  4. Good idea vipi kuhusu urasimishaji wa bidhaa kupitia TFDA yaani haya mamlaka yanapatikana wapi??

    ReplyDelete
  5. Nahitaji jua mahitaji mhimu kwenye duka la vipodozi

    ReplyDelete