Maisha ya utafutaji si mara zote kwamba yana mkwamo , kuna kukutana na mkwamo lakini wewe ukiwa mkubwa dhidi ya mkwamo basi hapo utakuwa na nafasi kubwa ya kuyafikia mafanikio makubwa na kuanza kuishi utajiri na utoshelevu kwa haraka sana.
Leo kwenye jukwaa lako pendwa la jikite na fursa nimekuletea dalili sita za kukuhakikishia kuwa utakuwa bilionea kama utaamua kuweka juhudi na jitihada za kutosha kufanyia kazi dalili hizo na kutokukata tama haraka nazo ni hizi.....
- Una malengo makubwa na upo kiwandani sasa kuyafanyia kazi.
Asikudanganye mtu , kinachowatofautisha watu baina ya huyu na yule ni malengo walijiwekea na kwa hakika wameamua kuyatimiza kwa hali yoyote iwe mchana au usiku na wewe kama unalo lengo na lengo hilo linazo sifa muhimu hitajika yaani lina mpango , mkakati , tarehe ya mwisho , na kusudi la kutaka kulifanya hakika upo kwenye wakati mzuri kuyaendea mafanikio makubwa na kuyapata kwa haraka , nikukumbushe falsafa moja ya kale isiyopitwa na wakati isemayo kuwa "ukiona kwa hakika hauwezi kulifikia lengo kamwe hata usibadilishe lengo bali badilisha mikakati na mbinu utalitimiza hakika".
2. Una uwezo wa kufanya maamuzi kwa haraka.
Wafanyao maamuzi bila kughairisha wana nafasi kubwa sana ya kukutana na fursa na kufanikisha kile wanachokitaka kwenye maisha yao , ikiwa nawe unayo hii tabia ya kufanya maamuzi sahihi kwa haraka basi una nafasi kubwa ya kuwa bilionea kwa hakika, Endelea kuboresha uwezo wako wa kufanya maamuzi na kutenda kwa haraka bila kujivuta vuta kwakua kufanya hivyo unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanikisha mengi bila kuchelewa.
3. Muda wako mwingi unatumia kuzungumza mawazo(ideas) na si watu.
Kila jambo duniani unaliona ambalo ni kwa matokeo ya mikono ya watu chanzo kikuu chake kimetokana na mawazo na kwa maana hiyo uwezo wako wa kuwa na mawazo kuna kusaidia kwa haraka kuziona fursa ama kuweza kuona ambayo wengine wanaita matatizo lakini wewe wayaona kama fursa na upo haraka kuyageuza kutoka matatizo na kuwa fursa , hii inamtaka mtu anayjihusisha na mawazo na si kuzungumza watu wakati wote , Kama ulikuwa haufanyi anza leo kuwa mtu wa kuzungumza mawazo na si kupoteza muda wako mwingi ukiwazungumza watu haina faida kwako.
4.Una sifa kuu ya un'gan'ganizi au kutokukata Tamaa.
Kutokukata tamaa ama kuishia njiani ndiyo njia kuu ya watu wengi kuwa kwenye vilele vya mafanikio duniani kote , na sifa hii hutokeza mafanikio ambayo kwa hakika kama ungeamua kuishia njiani usingeweza kupata ama kufanikiwa , kwahivyo ni muhimu sana kujenga sifa kuu ya kutokukata tamaa na badala yake tuendelee kujiboresha siku hadi na kwa maana hiyo tutakuza uwezo wetu wa kufanikiwa haraka tofauti na kama tutaka tamaa.
5. Unafanya moja kati ya haya matatu ama yote kwa pamoja Biashara , Kilimo au Teknolojia(Taarifa)
Ulimwengu umetoka mbali kwa kupitia vipindi mbali mbali lakini kuna mambo pamoja na dunia kupitia vipindi vingi yamebaki kuwa imara nyakati zote na yametokeza mafanikio kwa watu na watu wameanza kuona mwanga kutokana nayo na wametokea kuwa mabilionea kwa haraka sana na mambo hayo ni
a) kuwa na biashara.
Karne na karne biashara imekuwa eneo kuu la watu kufanikiwa na kuwa na utajiri mkubwa , Nawe kama unafanya jambo hili basi una nafasi kubwa sana ya kufanikiwa endelea kuikuza , kuiendeleza na kuiboresha kuendana na mahitaji ya wateja wako utaona mafanikio kwa haraka.
b)kufanya kilimo.
Kilimo ndiyo eneo kuu panapotoka bidhaa nyingi kwenda kwenye mrengo wa biashara na bidhaa hizo hakuna hata mtu mmoja huzipuuza kuzinunua iwe isiwe awe anaumwa au mzima atanunua bidhaa zitokanazo na kilimo hususani chakukula na mambo mengine , wito kwako boresha na kuza kilimo chako kwa haraka na anza kuyaishi maisha yako.
c)Kujihusisha na Teknolojia.
Hapo kale ilizoeleka kuwa kutajirika ni jambo linalohitaji muda mwingi kutokeza mafanikio lakini hali imekuwa tofauti kwenye karne ya 21 kwenye kizazi cha mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo vijana wengi kwa haraka sana wameingia kwenye ulingo huu na wameibuka wakiwa mabilionea kwa mfano mmiliki wa mtandao wa facebook ndugu Mark Zugerberg , kwahivyo na wewe kama wajihusisha na mambo haya una nafasi kubwa sana ya kufanikiwa na hapa nchini kwetu tunao mfano wa kijana kama Miladi Ayo na Isaya Yunge hawa wamekuwa kama taa kwako anza na wewe.
6. Hauweki jitihada zako kwenye utajiri wa kulala na kuamka ukiwa tajiri.
Vijana wengi kwenye ulimwengu wa sasa wanakabiliwa na njaa ya mafanikio bandia (fake success) kwamba walale na kesho waamke wakiwa matajiri kwa kupata utajiri kwa njia rahisi kabisa kama kucheza michezo ya kamari , kujihusisha na kubeti, kuomba dua wakati wote, na mengine kama hayo si njia kwa hakika ya kukufanya wewe uwe na mafanikio na kama wewe ni miongoni mwa vijana wasiofanya haya basi unayo nafasi kubwa ya kufanikiwa na kuwa bilionea.
Uwe na Usomaji Mwema , Mwandishi wa makala haya ni Mwanafunzi wa kudumu wa Maisha.
Michael The Great One Mwanagenzi (075 988 0010).
Pamoja sana kamukubwa
ReplyDelete