Kunyauka Sio Kufa - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Friday 5 January 2018

Kunyauka Sio Kufa

Habari za ijumaa wapendwa 
Kama ilivyo ada kwa wenzentu kwenda katika nyumba za ibada kumshukuru Mwenyezi Mungu leo tuingie kwenye mioyo yetu tuone imekufa baada ya kunyauka.
Katika hali ya kawaida mimea inapokumbana na dhoruba ya ukame na kukosa joto la kiasi na unyevuunyevu hunyauka ila mkulima anatengeneza mazingira ya kuufanya mmea usife kwani anatarajia kupata mazao ambayo ni kwa ajili ya chakula, dawa, mavazi na malazi ambayo yanatumika kila siku katika maisha yake hali kadhalika kuweka mazingira safi yatakayoleta mandhari ya kuvutia kuwezesha viumbe vingine kuweza kupata malazi na malisho.
Maisha yetu yamenyauka kutokana na matatizo ya kiuchumi, kiafya, jamii inayotuzunguka, kukosekana kwa fursa, elimu, na uwepo wa wataalamu na wasomi wasiotumia elimu yako kuisaidia jamii bali kumnufaisha mwajiri wake. 
Unyauko uliopo katikati yetu unaonekana katika biashara, kwenye ajira na kwenye uzalishaji wa kila mmoja wetu.
Changamoto za unyauko usiotunzwa na kutengenezewa mazingira bora hupelekea kutokea kwa changamoto zifuatazo katika maisha yetu ya kila siku:-
a) Msongo wa mawazo
Tumeendelea kuona ongezeko kubwa la milipuko ya magonjwa yasiyoambukizwa kama kupooza  (stroke),magonjwa ya moyo, matatizo ya figo, kisukari na blood pressure kwenye jamii kwa makundi ya wazee, watu wa makamo na vijana. Hali hii imekuwa tofauti na kipindi cha nyuma na imeendelea kukua kwa kasi huku watabibu wakiendelea kutumia jitihada kuokoa uhai wa wagonjwa hawa. Lakini anguko lao kunatokana na kunyauka kwenye ubongo kutokana na kukosa matunzo ya utatuzi wa changamoto zao.
b) Malezi hasi ya watoto 
Wazazi wengi wa leo wamekuwa na jukumu la kuhakikisha familia inapata malazi, chakula na mavazi bora kwa watoto lakini wanakuwa na malezi hafifu. Ni ukweli usiopingika kuwa wasichana wakazi ndio wamekuwa walezi kwa nafasi kubwa kwa baadhi ya watoto waliowengi. Baba/Mama anaamka saa kumi alfajiri anarejea nyumbani saa nne usiku kwa mwaka mzima muda wote anatafuta njia sahihi ya kuongeza kipato kuweza kuwasaidia watoto wake. Kuna haja ya kutengeneza muda wakujifunza kutoka kwa watoto wako ili tuepushe wimbi la ongezeko la watoto wasiokuwa na maadili katika jamii yetu.
c) Umasikini
Kuwepo kwa umasikini uliopitiliza ni kunyauka kwa fursa na kukosekana kwa wataalamu kwenye jamii. Tunaendelea kuona mdodoro wa uchumi kwenye nchi nyingi zenye uchumi wa chini na wakati na hususani nchi zinazoendelea( developing countries) hali hii inatokana na kiwango kikubwa cha umasikini. Wanajamii hawa wakitengenezewa mazingira ya kutokunyauka kifikra na kukua kifursa tutegemee kuona uchumi wa nchi hizo kukua namaendeleo ya mwanachi mmoja mmjoa kuongezeka.
d) Mmonyoko wa maadili na mfarakano wa familia 
Katika hali ya kushangaza tumeendelea kuona vijana wengi hususani walioko kwenye makuzi  (adolescents) kujiingiza kwenye mambo hatarishi kama utumiaji wa madawa ya kulevya na vilevi na wengine kujihusisha na matendo ya wizi. Hali hii inatokana na hali ngumu ya kiuchumi na kukosekana kwa ajira familia kuwa kwenye umasikini uliokithiri na kukosekana kwa malezi hali ambayo inampelekea kijana kujikita kwenye mambo hatarishi. Tumeendelea kuona ongezeko la malezi ya mzazi mmoja kwenye familia zilizo nyingi hali hii inachangiwa na kushuka kiuchumi na wazazi kujiingiza kwenye biashara zisizo halali na kupelekea kuikimbia familia kukwepa majukumu. Kama mmojawapo akupatiwa matunzo ya matibabu na kupewa njia mbadala ya kujikwamua na kunyauka alikonako atastawi nantutaendela kuwa na vijana na jamii yenye mchango katika taifa.
Hizo ni baadhi ya changamoto chache ambazo zinaweza kuhuishwa kutoka kwenye unyaoko kwenda kwenye kustawi tena na kutoa mazao yenye tija kwa mkulima na mtumiaji wa mwisho.
Tusikate tamaa tunapopata unyauko jikusanye jiunge na watu wengine omba ushauri washirikishe watu changamoto zako utaona ukitoka kwenye unyauko na kustawi tena. Hakuna anayetaka mmea wake ambao ni msukumo na matamanio ya kufanikiwa kwenye maisha yako uliko ndani yako unyauke hivyo kama ambavyo unapigania hali yako usiwe mchoyo kumsaidia na mwenzako afanikiwe kwa kumpatia njia sahihi na mawazo chanya yatakayomsaidia kukua kifikra na kuona fursa. 
Ahsante sana 

No comments:

Post a Comment