Mbinu zitakazo Kujaza Fedha Mwaka 2018. - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Monday, 1 January 2018

Mbinu zitakazo Kujaza Fedha Mwaka 2018.


Mwaka mpya na mambo mapya hizi ndizo sauti za washelekeaji wa mwaka mpya kwenye moja ya mtaa wangu hapa Buhongwa , Mwanza ilikuwa shamrashamra sana. Lakini pamoja na shamrashamra hizo unaweza kuwa mwaka huu ukafanana na mwaka tulioutoka kwa maana kama haukufanikiwa kwenye mambo yako mengi pia na mwaka huu unaweza usifanikiwe vilevile kama hauna Nyenzo yaani (MAARIFA SAHIHI)

Leo tutaangazia mbinu  zitakazokufanya uwe na fedha za kutosha kutimiza malengo yako.

1.USINUNUE KITU KWA KUSUKUMWA NA TAMAA.

Mara nyingi sana tumekuwa wanunuzi wa vitu ambavyo kwa Mara nyingi hatukuwa tumepanga kununua vitu hivyo lakini tumejikuta tunanunua tu na baadaye kuanza kujuta tukifika nyumbani kwamba kwanini nimenunua kitu hiki na huku nilipaswa kutimiza jambo Fulani , Mwaka huu kataa kufanya hivyo jiwekee mpango wa kuacha tabia hiyo Mara moja kwa kufanya haya
√Ukitaka kununua kitu jifunze kutengeneza orodha nyumbani ya vitu vya kununuliwa kwanza.
√ukiona unashawishika na kununua kitu hicho sogea pembeni kidogo kando na hicho kitu kisha vuta pumzi kubwa kisha jiulize hivi hiki kitu kinamchango gani hasa na kisitishe malengo yangu. 

2.JIWEKEE AKIBA YA TSH 10,000 KILA WIKI KWA AJILI YA KUSTAAFU.
Uwekaji wa akiba hii unakufanya uwe na Faraja ya kuona kesho yako ukihimili mambo usiyoyafahamu vyema na ujasiri wa hali ya juu , jifunze kutimiza lengo dogo kama hili hata kama utaweza kuweka Tsh 5000 weka usiache na usifungwe na kiwango hicho nilichotaja hapo juu lakini ni muhimu kuwa na mwanzo mwema kuliko kupuuza.

3. LIPA MADENI NA UJIEPUSHE KUKOPA SANA KUSIKO NA TIJA.
Kukopa ni jambo zuri sana lakini ni muhimu kufahamu kuwa fedha ya mkopo siyo Pesa yako bali ni Pesa ya yule uliyemkopa na utakaa nayo kwa kipindi kifupi tu na kisha utawajibika kulipa fedha hiyo kwa mwenye nayo , kwahiyo mwaka huu jitahidi kupunguza madeni yasiyokuwa ya lazima na jiwekee mpango wa kulipa madeni mengine.

4.JIFUNZE KUWEKA BAJETI.
Kuweka bajeti ya matumizi yako kutakusaidia sana katika kuwa na mwaka wenye mafanikio tele maana bajaeti hutumika kama kidhibiti mwendo , kwani kinakufanya usitumie fedha nje ya mpango uliojiwekea. Ni vizuri kujifunza kupangia matumizi fedha ama kipato chako. Mfano bajeti yako inaweza kuwa na mambo kama haya 
√matumizi ya nyumbani
√matumizi ya usafiri
√Matumizi ya matibabu
√Dharula
√Akiba
Na hata burudani.

5.ISHI KULINGANA NA KIPATO CHAKO.
Waswahili wanamsemo usemao "kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake mwenyewe"
Kuishi ndani ya kipato chako ni sawa na mbuzi kula kwa urefu wa kamba Yake.
Tania hii itakufanya kuepuka madeni yasiyo kuwa ya lazima.

Karibu sana na kheri ya mwaka mpya 

Ndimi Michael Charles 0759880010

No comments:

Post a Comment