Ukikaa chini ukawazua vyema wengi wanahitaji furaha kwenye maisha na wengi wanasema njia ya kuyafikia mafanikio ya kweli ni kuwa na furaha , kila mmoja kwenye jamii utasikia akisema natamani niwe na kazi nzuri , napenda niwe na Mme/mke mzuri , nyumba nzuri na kama mambo hayo hayatatimizwa kile kinachoitwa furaha kitatoweka na hapo hapo ni kweli hata kuwa na maisha mazuri si ndivyo?
JE NI MAMBO GANI HUWAFANYA WATU WAWE NA FURAHA YA KWELI?
Watafiti wa saikolojia wamegundua kuwa kukimbia jambo ama tatizo kumeongeza ukubwa wa watu kukosa furaha maradufu
Leo utaona watu wanavyojiua , nchini marekani ongezeko la watu wano jiua limeongezeka Mara dufu kwa mfufulizo wa miaka 30
Lakini hali ni niyakushangaza kidogo kuwa hats wale wenye maisha mazuri bado na wao hawana furaha bado wamebakiwa upweke , hofu , kutengwa n.k
Sasa basi ni mambo gani sasa yanachochea furaha ya kweli kama nao wenye maisha mazuri nao wanaendelea kukosa furaha.
FURAHA NI NINI?
Furaha ni hali ya ya kulidhika (comfort) na kujisikia vizuri kwa wakati , kama ndiyo hii maana ya furaha ni dhahiri kuwa kunahitajika jambo hususa kubwa zaidi juu ya hili tu la kuwa Na furaha Na jambo hill wataalamu Na watafiti wameligundua kuwa ni kuwa na Maisha yenye maana hiki ndiyo daraja linalowafanya watu wawe na furaha ya kweli kwenye maisha labda tujikite na fursa kufahamu ni nini maana ya Maisha yenye maana
Maisha yenye maana ni umiliki na uwezo wa kuhudumia Kitu Fulani kwa wengine nje na kujihudumia wewe mwenyewe na uwezo huu hukua kuanzia ndani yaani ni hitaji la ndani yako.
Wale wenye maisha yenye maana ndiyo wale wenye furaha ya kweli , hawa hufanya kazi zao vyema , hutimiza malengo yao , shuleni hufanya vizuri na hata kwenye uongozi huchochea ukuaji ziadi.
SASA TUNAWEZAJE KUISHI MAISHA YENYE MAANA?
Baada ya utafiti wa miaka mitano wa binti Emily Estafahami Smith , amekuja na nguzo nne za kuwa na maisha yenye maana
1.UMILIKI
Umiliki huja pale unapokuwa kwenye jamii thamani yako, utu wako , na mchango wako unadhaminiwa na wewe pia kudhamini michango na thamani ya wengine bila kujali wanaotoa thamani hiy o ni wale unaowapenda tu lakini iende kuthamini mambo kutoka hata kwa usio wapenda Bali una upendo na kile wanalicho nacho kama binadamu , kulifanya jambo hili liwe bora kwako na uuanze kuishi nalo jitahidi kujenga upendo , upendo ni daraja la kuwainua nyinyi nyote kwenye jamii.
2. KUSUDI.
Kutafuta kusudi lako la kuwepo duniani ni tofauti na kutafuta kazi itakayokupatia furaha kwanini ? Kusudi ni kile unachotoa zaidi si unachotaka zaidi , kwahiyo ufunguo wa kufahamu kusudi lako hapa duniani ni ule uwezo wako wa kuwahudumia wengine, hii inaonyesha dhahiri hata ukiwa kazini ile namna ya mchango wako unavyohitajiwa ndiyo kusudi lako hilo.
Kusudi huwa halitafutwi ili likufanye uishi Bali kusudi hukitafutia Kitu ili uishi.
3.KUTOKUWA NA MIPAKA KATIKA KUFANIKIWA.
Ule uwezo wa kuchukua fursa na kuzifanyia kazi na kutokuona hali ya kutokuwezekana kwa mambo Bali kuona njia kwa kila jambo huku ukijiunganisha na nguvu kuu na kubwa Katika kuyatimiza unayohitaji , kuna Rafiki Yangu anaitwa Wendy George Chomola yeye kuna kipindi alikuwa akiiumwa sana kichwa kinamuuma sana sana , na alikaa kwa kipindi kirefu kichwa kikimsumbua alikwenda hospitalini wakamuongezea masharti badala ya tiba wakamwambia kwa maumivu ya kichwa chako unapaswa usicheke sana na kukasirika sana , mzigo mkubwa. Lakini Siku moja alijiaambia siwezi tena kuendelea kuugua kichwa Mara kwa Mara ni kininyime raha kupitia kauli ile na kukataa ugonjwa Wendy alipona kichwa na haujaumwa tena kichwa cha namna ile na wewe unaweza usiweke mipaka kwenye Maisha yako utakisia mwingine anasema "sisi ni wa hivi hivi" endelea kuwa wa hivyo hivyo hakuna wakuja kutaka usiwe wa hivyo hivyo.
4 MSIMULIAJI WA HADITHI.
Unaweza kushangaa kidogo kwanini niwe msimuliaji ndiyo niwe na Maisha yenye maana , wewe ni hadithi na uzuri wa hadithi hii inaweza kusimuliwa na wewe ukijiambia wewe mwenyewe , nyakati nyingi tumesahau kuwa sisi ni sehemu ya waandishi kwenye hadithi zetu ,na uzuri wa hadithi zetu tunaweza kusibadilisha kutoka kwenye hadithi mbaya mpaka hadithi nzuri kwa kuediti tu , kuhariri na kisha kujisimulimulia wenyewe.
Furaha ni jambo linakuja na kupita lakini Maisha yenye maana ni jambo la muhimu sana kuwa nalo
Michael Charles 0759880010.
No comments:
Post a Comment