Njisi ya kutambua thamani yako na kudai Stahiki Yako. - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Tuesday 26 December 2017

Njisi ya kutambua thamani yako na kudai Stahiki Yako.


Mara nyingi wengi Mwa watu waliojiajiri ama kuajiriwa wanapitia wakati mgumu sana kufahamu thamani ya kile wanachokifanya na je wanalipwa stahiki ambayo inaendana na kile wanachofanya kwenye kazi ama eneo walipo jiajiri fuatana nami kujua thamani yako.

Kuna maswali muhimu unayopaswa kujiuliza na kuyapatia majibu na ukisha kuyapatia majibu hapo ndipo utakapo fahamu thamani yako.

Miongoni Mwa maswali hayo ni haya ...

1. Ni jambo gani wahitaji wangu wanataka toka kwangu?
Swali hili linajenga taswira ya kile unachotoa kwa wahitaji wako awe Boss wako ama wateja wako kuwa je kile ninachowapatia ndiyo kile wanachohitaji , ni rahisi sana kufamu mwajiri / mteja wako anahitaji nini toka kwako na jibu rahisi ya swali hili wahitaji wako wanahitaji huduma bora toka kwako. Ukisha kufahamu wanahitaji huduma bora toka kwako na rahisi sana sasa kwako kujipanga na kuamua kuwapatia huduma iliyotukuka na kuweza kufikia uhitaji wao na kukufanya sasa ujue unaweza vipi on a thamani yako kwako na vipi unaweza dai ulipwe kulingana na thamani unayotoa.

2. JE NI UJUZI GANI WA PEKEE NINAO AMBAO UTANIFANYA KUFANYA VIZURI KUKUTANA NA MAHITAJI YA WAHITAJI WANGU?
Ni vyema kama mjasiriamali aliyebobea ukafahamu uwezo ulio nao ambao unakufanya uwe tofauti na wengine na inapotokea boss /wateja wako wanataka jambo Fulani lifanywe kwenye ajili zao Mara jina lako litokee kuwa jambo hili anaweza kulifanya vyema sana ndugu wewe   na hapo utakuwa na nafasi nzuri ya kujisukuma kwenda mbali zaidi na umuhimu wako ukionekana hiyo ni thamani yako inachipua tena kwenye ubora wa kiwango cha juu.
Kutimiza hili usiache kujifunza ujuzi mpya kila kukicha hiyo ndiyo uwe ngao yako.

3.NI MATATIZO YAPI NIMEYATATUA KUTOKA KWA WAHITAJI WANGU?
Uwezo wa kutatua changamoto nyingi na kwa kiwango cha juu na ubora wa hali ya juu ndiyo unaokufanya wewe uwe wa thamani sana sana na kwa maana hiyo lazima ujiulize ni matatizo yapi nimeyatatua kutoka kwa wahitaji wangu yaani Bosses/ na wateja wangu , ukishafahamu matatizo hayo uliyotatua inakupa Uhuru wa kujua thamani Yangu ina umuhimu wa kuhitajiwa na unaweza kudai stahiki yako kulingana na thamani unayoitoa.

4. NI THAMANI GANI NIMEWAHI KUIONGEZA?
Kwenye kazi yako ama kwenye biashara yako yako mapungufu mengi ambayo huenda wengi unafanya nao kazi hawajayaona , kama umeyaona ni wajibu wako sasa kuyaondosha mapungufu hayo na kadili unavyoondosha matatizo hayo ndiyo unaongeza thamani Mara dufu kwako na kwa kazi yako na utakuwa wa kuhitajiwa.

NINAWEZAJE KUTIMIZA HAYO?

Ni muhimu kutambua vikwazo vinavyokufanya usitimize mambo hayo na vikwazo vikubwa ni Hofu & Woga tambua kuwa kama utaruhusu Hofu & Woga vikutawale hivyo ndivyo vinavyochukua thamani yako bila Hofu &Woga toka kwako.

Ondosha Hofu na uoga kwa kutumia mbinu hizi tu 

√ Iambie akili yako Woga na hofu ni sehemu ya maisha 

√ Iambie akili yako Woga na hofu havituambii nini thamani yetu

√ Iambie akili yako wajibu wangu ni kutoa huduma iliyotukuka na kuongeza thamani na hii itanifanya kuwaza pakubwa.

Iambie akili yako lazima nijifunze kukipenda kile ninachokifanya hapo ndipo thamani Yangu itaonekana wazi.

              MWISHO.


Uwe na siku njema  wasiliana nami MICHAEL CHARLES 0759880010.

No comments:

Post a Comment