Mbinu muhimu za kuendesha maisha - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Tuesday 26 December 2017

Mbinu muhimu za kuendesha maisha



Habari za wakati huu mpendwa msomaji wa blog ya jikite na fursa
Natumai umzima wa afya ukiendelea na harakati za kimaisha kuhakikisha mkate unakwenda kinywani ..
Leo tunakwenda kuzungumzia kuhusiana na mbinu muhimu za kuendesha maisha , Mara nyingi miongoni mwetu hushindwa kufanya kile kilichosahihihi kwa kuwa na visingizio vingi lakini ukweli ubaki pale pale kuwa kama hauna maarifa ya jambo lolote tegemea Matokeo yasiyolidhisha kwa hatua unazoziendea.

MBINU MUHIMU ZA KUENDESHA MAISHA.

1. HATUA NDOGO HUWA HATUA KUBWA.
Ukitaka kwenye maisha yako kufanya jambo kubwa hakikisha unajifunza kufanya hatua ndogo ndogo hizo zitakufanya kuweza kufanya na kutimiza mambo makubwa kuna falsafa inasema "mambo madogo madogo ndiyo huleta tofauti kubwa" kwa hivyo amua kujikita kufanya madogo kwa usahihi pia makubwa utakuwa na uwezo nayo.

2. JIFUNZE KUJIWEKEZA KWAKO MWENYEWE.
Fanya Kitu kwa ajili yako , jipe ofa mwenyewe , Fanya kazi kwa juhudi kisha nenda matembezi hii itaongeza morali kwako na kukupa motisha zaidi.

3. WEKEZA KWA WENGINE.
Fanya kitu cha thamani kwako , wasaidie kwa kufanya haya ...
√ Wapende wao zaidi na zaidi ukishawapenda wao watakujibu kwa wema zaidi kama utawauliza Kitu na hapo utaweza kupata vitu kutoka kwao na Mara moja utakuwa umefanikiwa.

4. HAUHITAJI ALAMU KUAMKA KWA SASA.
Kuna watu wengi sana wanapenda kuamshwa kwa kutumia alamu ili aweze kuamka lakini Kuna mbinu bora sana ya kukufanya uamke mapema bila kuamshwa kabla ya kwenda kulala kunywa grasii mbili za Maji utaamka mapema sana.

5. TUMIA KIDOGO KULINGANISHA NA KILE UNACHOPOKEA.
Usiwe mtu wa kujisahau kwenye matumizi ya fedha kwa kutumia kiwango kinachozidi mshahara wako hali inayokupelekea hadi kukopa fedha toka kwengine , jifunze kuweka akiba na kujibana kwa ajili ya baadaye maana Leo unafahamu vyema upo na afya lakini haufahamu kesho.

6.KUTABASAMU NI SUMAKU YA KUVUTA MENGI MAZURI.
Kwenye tabasamu ndipo palipo na ubunivu , ndipo palipo na fursa jifunze kutabasamu kutakusaidia sana kuvuka kwenda mbali zaidi na afya yako itaimarika Mara dufu.

No comments:

Post a Comment