Kuwalea watoto wa kiume na kike Vyema - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Wednesday, 27 December 2017

Kuwalea watoto wa kiume na kike Vyema


Kumekuwepo na maneno mazuri sana kuwahusu watoto wengine utawasikia wakisema watoto ni zawadi , watoto ni malaika na mengine mengi kama hayo na ni jambo la heri na busara kufahamu watoto ni zawadi na hata wao kuwa malaika 

Unapopata Mtoto ama watoto ni fursa nzuri ya kuanza kujenga jamii ya baadaye yenye kutegemeka ama isiyotegemeka ama wengine wanasema rasirimali chakavu  uchakavu huo ama ubora huo unachangiwa na asilimia kubwa na sisi wazazi tunao amua kuwalea watoto hawa 

Leo tujike na fursa ya kufahamu ni namna gani tunaweza kuwalea watoto wetu wa kiume na wakike ambao watakuja kuwa wenye kutegemeka.

MAKOSA TUNAYOFANYA:-
√ Hatutaki kukubali kuwa watoto wa kike kwenye ubinti wao wanapendeka sana kuliko watoto wa kiume.

√Hatutaki kuwaambia watoto wetu uhalisia wa maisha na kuwapa mbinu kama kuweka malengo kwenye maisha yao n.k

√Tunapenda kuwashinikiza watoto juu ya shule na mitihani tu wakati kwa uhalisia maisha hayahitaji shule na mitihani toka mashuleni kwao zaidi ya shule ya nyumbani.

√ Kuwapatia vitu badala ya kuwapa muda pamoja nao 

NINI SURUHU YA HAYO.

Kufahamu wapi umekosea ni njia salama sana kukupeleka kwenye kufahamu njia na suruhu ya tatizo husika , zifuatazo ni njia zinazoweza kuwasaidieni muwe walezi wema kwa watoto 

1.Chakula chenye virutubisho na cha kutosha.
Vyakula ndiyo pendekezo la kwanza la mzazi mwema kwa watoto wake na hii wengi wamejaribu kuikwepa na wanakwepa hapa ndiyo chanzo cha watoto wengi kupoteza dira ya kule waendako , kwenye chakula ndimo palimo na uhai , Ndimo palimo na akili. Kwahivyo dumisha upatikanaji wa chakula nyumba na si vyakula tu Bali vyakula vyenye virutubisho vyote.

2.Mazingira salama na safi.

Mazingira ya nyumbani ni darasa tosha kwa watoto wako juu ya kuwa watu wenye kutegemeka binti aliyelelewa kwenye familia inayojali usafi wa mazingira ni binti ambaye ataendeleza jambo hili kokote aendako vivyo hivyo hata kwa yule aliyekulia kwenye familia inayohusudu uchafu naye atadumisha mila ya uchafu kokote aendako , lakini pia usafi unaepusha mengi wadudu waharibifu na waletao magonjwa n.k kwahivyo ni muhimu kudumisha usafi wa mavazi , malazi itapendeza sana.

3.Jenga utamaduni wa kushiliki kazi za nyumbani na watoto wako.
Jambo hili litaongeza ujuzi mpya kwa watoto wako , kamwe usiache kuwapatia kazi za kufanya watoto wako na wakati mwingine shiliki nao kazi hizo , na hakikisha kila mmoja anajisikia vyema kushiliki kazi hizo kwa kuwa mbunivu zaidi kwamba wakimaliza kazi hizo watapokea bakishishi kama asante ya kufanya kazi vyema ama hongera kwao kwa kuwa wema na kazi.

4. Pendelea kuwauliza maswali yenye kuwachochea kutafuta majibu yenye maana.
Unapokuza watoto unawajenga viongozi wa baadaye wenye jukumu la kuongoza maisha yao ,jamii zao na hata kukuongoza wewe kwenye mapumziko yako ya uzee sasa ni muhimu kuwajenga watoto hawa kwa maswali bora ambayo yatawafanya kujenga uwezo wao wa kujieleza kwa mfano unaweza muuliza Mtoto wako baada ya kutoka shule , Vipi siku yako Leo shule ilikuwaje? , Nini kimekufurasha sana na pia hata kipi kimekuudhi mwanangu?

Mtoto atajisikia Faraja kwamba kuna watu wanajali mwendo wake popote anapokwenda.

5.Jifunze kwa hakika majibu yao.

Kuna wazazi anauliza jambo kwa Mtoto kisha anakwenda chumbani na kugunaguna tu hii haionyeshi hata kidogo kama kuna mawasiliano baina yako na Mtoto huyo. Kama sikiliza onyesha mwitikio kwa Yale unayoambiwa na Mtoto wako

Uwe na siku njema .....karibu tena 

MICHAEL CHARLES 0759880010.

No comments:

Post a Comment