Niwekeze wapi ? - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Monday 18 December 2017

Niwekeze wapi ?



Habari ya muda huu msomaji wa blog ya jikite na fursa ? Natumai u mzima.

Karibu tena kwenye darasa huru la fursa leo tutaangazia Jambo muhimu kuhusu uwekezaji nalo ni 

Niwekeze wapi ? Kwenye mtililiko wa fedha ama kwenye ukuaji wa mtaji ( capital gains) ? 

Watu wengi huwekeza kwenye mitaji inayokua yaani capital gains lakini matajiri na watu wenye maarifa ya uwekezaji huwekeza kwenye mtililiko wa fedha yaani (cash flow) uwekezaji kwenye eneo hili huwa ni wa uhakika kwakua eneo hili huwa na kasi kubwa ya uingiaji wa fedha 

Kwanini ? 
Kuwekeza kwenye mitaji inayokuwa ni sawa na kucheza kamari kwakua ukiwekeza huko unaanza kuwa na Tumaini kuwa fedha Yangu itaongezeka ,   kwa mtazamo huo ni dhahiri utakuwa hauna uhakika wa jambo hilo kuwa litatoa matunda lini

Kwa mfano anayenunua nyumba na kuwazia kuwa ataiuza kwa bei kubwa hapo baadaye wazo hili ni jema sana lakini tatizo linakuwa  HAJUI NI LINI ATAUZA NYUMBA HIZO  kwakua Mara nyingi nguvu ya soko huamua kuna kushuka na kupanda kwa bei 

Lakini huyu wa pili ambaye anawekeza kwenye fedha inayoingia kwa mfano ananunua nyumba kwa fedha za watu wengine na kupangisha wapangaji na kuanza kukusanya KODI  kila mwezi na hiyo hugeuka kuwa asseti. 

Mpaka hapo  sasa utakuwa umepata  mwanga wa mahali gani uwekeze kwenye mtililiko wa fedha ama kwenye mitaji inayokuwa ?

Nyongeza ya maarifa zaidi.

TUMIA MADENI NA KODI KUUPATA UTAJIRI.

•Matajiri hawakopi fedha ( KUTENGENEZA DENI ) kwa mfano kwa kununua TV ama kwenda kutembelea mbuga za wanyama kwa mkopo..

•Wao hutumia madeni kujenga utajiri anakopa na kununua nyumba ya kupangisha.


Karibu sana....

No comments:

Post a Comment