Kanuni tatu za kupata Fedha. - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Monday, 18 December 2017

Kanuni tatu za kupata Fedha.


Kila siku iendayo harakati za kutafuta na kumiliki fedha zimekuwa ndiyo jukumu la msingi sana kwa baadhi ya watu wanaojua nini wanataka na nini hawataki ulimwenguni hapa 

Pamoja na juhudi hizo kuna wengine wameishia kukosa mbinu mahsusi za kuwafanya waweze kupata na kumiliki fedha kama na wewe ni miongoni Mwa hao usitie shaka Leo tutajaribu kuangazia njia tatu muhimu za kukufanya upate fedha na uzimiliki.

NJIA HIZO NI ZIPI? 

Njia hizo ni zile ambazo zimekuwa maarufu sana masikioni mwetu lakini kwa kua ya kutokujua ama kuupuza tumekuwa hatuzitilii maanani njia hizo ni:-

a). KUOMBA.

Mtu yeyote anayehitaji kumiliki fedha ni lazima achukue hatua kadhaa ambazo na ni vyema ukafahamu kuna tofauti kubwa kati ya Kuomba na kuomba-omba , Kuomba ni njia ya kutaka jambo kutoka kwa wenye mafanikio ya jambo hilo , na kisha wao kukupatia ama kutokukupatia na jambo hilo linaweza kuwa maarifa ama usiadizi wa jambo husika sasa hapa ukikaa kimya utakufa maskini. 
Lakini kuomba-omba ni kitendo unachokifanya kwa kuhitaji jambo kutoka kwa watu hata wasio na mafanikio ya jambo hilo kwa lugha nyepesi unacheza kamari ya maisha maana unaweza kumuomba hitaji Fulani na wakati huohuo unayemuomba naye anauhitaji wa jambo hilo kwa ufupi utaambulia matusi.

Mifano ya watu waliotumia mbinu hii kufanikiwa ni pamoja na ......

1. Rais wa sasa wa marekani (Donald Trump ) yeye alimuomba babaye mtaji wa kibiashara na baba Yake alimpatia na kutoka hapo amekuwa ni mtu Mwenye mafanikio makubwa duniania kwa kupitia njia ya kuomba tu.

2. Mwanzilishi wa Facebook ( Mark zugerberg) 

Yeye alipopata wazo la kuunda Mtandao wa kijamii alimtafuta kijana Mwenye nafasi nzuri ya kipato na kumuomba amsaidie fedha zitazosaidia kuanzisha Mtandao huo ama kuendeleza wazo lao na bila hiyana kijana huyo kutafakari na kuona manufaa ya mbeleni alikubali kutoa usaidizi wa kifedha na Mara moja mtandao huo ulinza bila tatizo.

b). KUTAFUTA.

Hii ni njia ya pili ya kupata na kumiliki fedha nayo ni kitafuta , ni vyema kwa mfano umetumia njia ya kwanza kisha ukapata fedha unapaswa kuchukua hatua ya kuanza kutafuta kwakua kibachotafutwa hakijulikani kilipo sasa anza kuzitafuta fedha mahali zilipo ama zinakopatikana na kamwe hata siku moja usitafute Pesa kwa watu unaofananan nao kiuchumi kwani kila ukienda kutafuta fedha kwa hao utaambiwa "sina!"
Ni vyema kuzitafuta mahali zilipo na hakika ukitafuta bila kuchoka utazipata ziwe zako.

c). KUBISHA /KUULIZA 

Kwenye ulimwengu wa Leo kila jambo limerahisishwa sana hata ukitaka kufahamu njia anuai za kupata fedha jifunze kuuliza ama kubisha mlango ufunguliwe ili nawe uwe na nafasi ya kuingia ndani ili kuchukua na kumiliki fedha , Kwahiyo jifunze kuuliza juu ya mambo ya fedha nawe utapata majawabu yakulidhisha na ya kukufanya upige hatua ya juu zaidi kifedha.

Asante sana kwa kusoma fanyia kazi njia hizo.

MICHAEL CHARLES (0759880010)

2 comments: