Fursa Zitokanazo Na Ufugaji. - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Wednesday, 13 December 2017

Fursa Zitokanazo Na Ufugaji.



Zifutazo ni BAADHI tu ya fursa ambazo zinapatikana katika sekta ya mifugo na mnyororo wake wa thamani. Jipimie inayoweza kukufaa zaidi na uifanyie kazi katika kujitanua kibiashara na kujiongezea kipato chako. Zipo zinazohitaji mtaji mkubwa,unazoweza kuanza hata kwa mtaji mdogo, zinazotaka taaluma na zingine la hasha, nimekuandalia 20 kwa sasa, karibu uzipitie.

 1. Kutoa mafunzo ya ufugaji kwa malipo kwa wafugaji kupitia semina na madarasa mbalimbali.

 2. Kutoa huduma ya tiba majumbani yaani matibabu-mkoba (veterinary ambulatory services).

 3. Kutoa huduma za vipimo vya kimaabara.

 4. Kutoa huduma za ushauri na usaidizi (consultation) kwa njia ya moja kwa moja (ofisini kwako) au kwa kupitia mitandao ya kijamii.

 5. Kuandaa makala zinazohusu ufugaji na kuziuza kwa wenye blogs na websites zinazohusu masuala ya ufugaji.

 6. Kuandaa maandiko ya miradi (business/project plans) inayohusiana na miradi mbalimbali ya ufugaji.

 7. Kufanya biashara ya kununua sehemu moja na kwenda kuuza sehemu nyingine wanyama hai kama vile kuku, nguruwe, ng’ombe, sungura, n.k

 8. Kufanya biashara ya kununua sehemu moja na kwenda kuuza sehemu nyingine mazao mbalimbali ya mifugo kama vile mayai, maziwa, nyama, ngozi, n.k

 9. Kusindika mazao ya mifugo kama nilivyoyataja hapo juu ili kuyaongezea thamani sokoni.

 10. Kufanya biashara ya kuchinja mifugo na kuuza nyama.

 11. Kufanya biashara ya usafirishaji katika sekta hii.

 12. Kuuza madawa ya mifugo na vifaa tiba vingine.

 13. Kuuza vyakula na virutubisho vingine vya mifugo.

 14. Kuuza zana mbalimbali zinazohitajika katika shughuli mbalimbali za kila siku za ufugaji mfano gumboots, sprayers, mashine za kukamulia maziwa, vitotoresheo, n.k

 15. Kufuga kibiashara mifugo inayoliwa na isiyoliwa kama vile ng’ombe, mbuzi, nguruwe, kondoo, sungura, simbilisi, kuku, bata, kanga, kwale, njiwa, mbwa, paka, farasi, ngamia, n.k na kuwauza.

 16. Kutoa huduma za ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayohusiana na ufugaji kama vile mabanda bora, majosho, machinjio, mabwawa, n.k

 17. Kuandaa vipindi mbalimbali vya redio na televisheni vyenye maudhui ya kuelimisha juu ya ufugaji.

 18. Kuanzisha na kuendesha “YouTube channel”, blog au website zinazohusu masuala ya ufugaji (kwa lugha ya nyumbani yaani Kiswahili).

 19. Kuzalisha hydroponic fodder, silage, majani (pasture production) kwa ajili ya chakula cha mifugo na kuuza.

 20. Kuzalisha na kuuza mbolea (organic) na viwatilifu kutokana na taka zitokanazo na wanyama (samadi, mabaki ya vyakulaa na mkojo) kwa ajili ya kurutubisha ardhi inayotumika kwa kiimo cha mazao.

source JF

No comments:

Post a Comment