TABIA TANO ZA WAFANYAKAZI AMBAZO NI SUMU KAZINI. - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Thursday 25 January 2018

TABIA TANO ZA WAFANYAKAZI AMBAZO NI SUMU KAZINI.


1.WAPIKAJI NA WASAMBAZAJI WA MAJUNGU.
Tabia ya kusema vibaya , dhidi ya wafanyakazi wenzako , ama wateja inajenga taswira mbaya na kuharibu uhusiano wa karibu baina ya wafanyakazi wenzako na kupekelea kutokuaminiana kwenye kazi kama unaona una tabia hiyo acha Mara moja.

2. WALALAMIKAJI KUHUSU KILA KITU.
Yeye ni kulalamika kwa kila kitu na kwa wakati wote mpatie kazi fulani ni kulalamika tu  , mfanyakazi wa aina hii Mara nyingi huwa mvivu mvivu na anatumia kinga ya kulalamika kama ngao yake.

3. WANANGALIA FEDHA TU.
Yeye huangalia fedha tu mfanyakazi wa aina hii ni sumu mbaya sana inayoweza kuua kazi mapema sana na kuleta madhara makubwa kwa kazi yenu.

4.WANAHITAJI USIMAMIZI WA MOJA KWA MOJA.

Hawezi kufanya kazi kwa upekee wake kila muda anataka apewe usimamizi , ukiondoka tu naye anaondoka , unakuta hataki kujielemisha kuyajua na kuyafanyia kazi majukumu yake kwa wakati , mpaka asimamiwe.

5. HAWAKUBALI MAJUKUMU YAO.
hakuna asiyekosea , na usije ukafukuza kazi mfanyakazi kwasababu kakosea kila mmoja wetu hukosea , lakini mfanyakazi anapokesea anakataa kuhusu alichokosea sasa hapo ndiyo atazua sokomoko kwenye kazi maana atakuwa anakosea nyakati zingine kwa makusudi kwakua anajua atakataa.

Ni muhimu sana kubadili namna tunavyoenenda katika kazi zetu haswa namna tunavyofikiri na kutenda.

No comments:

Post a Comment