Tunapoelekea kumaliza mwezi wa kwanza katika mwaka 2018 leo ni siku ya 14 katika mwezi huu kuna watu bado wako kwenye machungu ya mwaka 2017 ambayo yanatokana na watu wanaowazunguka matatizo kwenye jamii na kukata tamaa.
Tukiangalia miongoni mwetu unaishi bila kujua thamani ya uhai wetu. Watu wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na uhai wa mtu binafsi ndio maana tunaendelea kuona wanajamii wakiendelea kupambana na msongo wa mawazo kutokana na mambo yanayofanywa kwao kutoka kwa watu wanaowazunguka.
1. Maeneo ya Kazi
Hali ya watu wengi kwenye maeneo ya kazi inakatisha tamaa na kurejesha nyuma thamani ya uhai wa watu wengi. Tunaendelea kuona watu wengi wakiacha kazi wengine kujikuta kwenye mahusiano na wakubwa wa kazi ili kuwa na Amani kwenye maeneo yao ya kazi watu wanajihusisha na mambo ya kishirikina ili kupata vyeo kwenye maeneo ya kazi.
Thamani ya uhai wako ni kuishi kwa kutekeleza majukumu yako na kuamini katika kila unachokitenda ili kurejesha na kuhuisha thamani ya uhai wako kuepusha mwili wako na magonjwa yashinikizo la damu na magonjwa mengine yanayotokana na msongo wa mawazo.
2. Kwenye maeneo ya shule/vyuoni
Watoto wetu wamekuwa wakipata changamoto za (bullied )kuzomewa, kukataliwa kwenye urafiki hata kushirikishwa kwenye mambo ya kijamii kutokana na kuwa na mapungufu machache au kushindwa kufanya mambo wengine wanayoyafanya.
Hali hii inapelekea watoto wengine kutamani kujiua au kufeli kwenye masomo na wengine kuacha shule na kujiingiza kwenye mambo ya kutumia vilevi na mihadarati ili kujiweka mbali na mambo ambayo yanawakosesha amani na kujiona hawana thamani ya kuendelea kuishi na kufurahia maisha na uhai waliopewa na Mungu
3. Mahusiano
Maisha ya mahusiano yameendelea kuwa na changamoto nyingi kila kukicha na watu waliokuwepo kwenye mahusiano wamekuwa hawaridhiki na walionao kwenye mahusiano na kujikuta kutamani kuwa na mahusiano mengine na watu wengine na kupelekea kuwafanya wale walioko kwenye mahusiano kujiona hawana thamani ya kuendelea kuishi na kujikita katika ulevi wa kupindukia au kujihusisha na mahusiano ya mtu zaidi ya mmoja wakiamini watapata furaha na kuona thamani ya maisha yao kwenye mahusiano hayo mapya.
Ukiangalia maeneo hayo matatu ndio maeneo makuu ambayo yanasababisha watu wengi kujikuta wanakosa kuhuisha thamani ya uhai wao na kuona hakuna sababu ya kuendelea kuishi.
Uhuishaji wa uhai unaletwa na mapokeo ya mambo yanayopelekea kukosekana kwa amani katika maisha yetu.
Jenga mazoea ya kuwa na furaha na kupokea kila tatizo kwa mtazamo chanya ambao ni endelevu.
Tengeneza tabia ya kuwa na furaha muda wote na hata ukiwa na hasira isidumu. Furaha inatengenezwa kwa kupuuza mambo na kuyachukulia mambo kwa wepesi na kuona hakuna umuhimu wa kuendelea kuchukulia mambo yanayokukosesha furaha kwenye maisha yako kwa uzito.
Tengeneza mazingira ya kupokea changamoto zozote zinazotokea kwenye maisha kwa muono mpana ambao utakupa matokeo chanya kwenye kila hali.
Weka pamba masikioni na maji mdomoni hii itatengeneza mazingira ya kutokusikia na kutokujibu kila utakachokisikia kiwe kina mapokeo chanya au hasi hii inakusaidia kuhuisha uhai wa maisha yako hata pale ambapo umekata tamaa na kuona huhitaji kuiona kesho yako.
Jipe muda kukaa mbali na mazingira na watu watakaoleta matokeo chanya kwenye maisha yako haijalishi hayo mazingira yanaumuhimu kiasi gani au hao watu wanaumuhimu kiasi gani ila kuna muda unapojiweka mbali nao unahuisha uhai wa maisha yako ambao unaweza kuudumisha kwa kufanya maisha hayo ya kujipa muda kuwa endelevu au kuisha kwa kipindi kifupi.
Jenga muda wa kufanya mambo yanayofurahisha watu wengine ili kujiona unathamani kwa watu waliopokea msaada kutoka kwako. Muda mwingine furaha za maisha yetu ni kuona watu wengine wanafurahishwa na matendo ya maisha yetu.
Ahsante sana kwa kuwa nami
No comments:
Post a Comment