Tanzania Tujifunze Kilimo Biashara Kutoka Congo DR - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Monday, 11 December 2017

Tanzania Tujifunze Kilimo Biashara Kutoka Congo DR


Serikali ya Congo DR imeanzisha mpango kabambe katika kilimo ambao ni Tumaini jipya na kupigiwa mfano barani Afrika hushsani nchini kwetu Tanzania na mpango huu unatatajiwa kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi , kijamii na kisiasa nchini Congo DR.

Mpango huo unajulikana kama agro- industrial park, unalenga kuanzisha mashamba makubwa yenye ekari elfu hamsini 50,000 hadi laki moja na hamsini 150,000 kwa kila mkoa kwa ajili ya kuzalisha Mazao ya chakula 

Lengo la mpango huu ni kuhakikisha usalama wa chakula , kutengeneza ajira kwa vijana na kuokoa takribani dola za kimarekani bilioni 1.5 ambazo serikali ya Congo hutumia kila mwaka kuagiza chakula kutoka nje ya nchi hiyo.

Mpango huo utatekelezwa kwa ushilikiano wa makampuni ya ndani ya Congo DR , ambapo serikali ya Congo itatoa ardhi kwa wawekezaji ambao watatumia ardhi hiyo kuzalisha nafaka , mboga mboga kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi.

Tayari hadi sasa serikali ya Congo imewekeza dola za kimarekani milioni 100 katika moja Shamba lililopo kilometa chache kutoka mji mkuu wa Kinshasa kwa ajili ya miundombinu wezeshi kama vile barabara, umeme, na Maji 

Sehemu ya matunda ya mpango huo mpaka sasa tayari ekari elfu tano zimelimwa na katika Shamba la ekari elfu moja vijana wanapanda aina mbalimbali za mboga mboga 

Mradi huo unataraji kuleta neema kubwa nchini ni humo ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa vituo vya maendeleo ya kilimo vitakvyokuwa na mashamba ekari mia mbili mpaka mia tatu  kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakulima wadogo wadogo nchi nzima pia maeneo ya mradi vitajengwa Viwanda vya usindikaji Mazao, maghala ya kuhifadhia Mazao , vituo vya usambazaji na makazi ya wafanyakazi.

Ni wakati muafaka sasa kwa nchi yetu pia kunifunza jambo hili na kulianzisha hapa nchini kwetu kwani kwa kiasi kikubwa litaleta manufaa makubwa kwa nchi yeti.

No comments:

Post a Comment