Mafanikio ni safari isiyo na mwisho. - JIKITE NA FURSA

Latest

Fursa mbalimbali za kukuinua kiuchumi

Tuesday, 12 December 2017

Mafanikio ni safari isiyo na mwisho.



Watu wengi wanapoyafikia mafanikio huwa wana nafasi kubwa sana ya kushindwa na moja ya sababu zinazowafanya washindwe , wao hufikiri mafanikio yana njia moja tu kuyafikia mafanikio 

Lakini mwanzo wakati unayatafuta mafanikio huwa tunafanya kila kitu kuhakikisha tunafikia mafanikio hayo na jambo zuri huwa tunayapata mafanikio na baada ya kuyapata mafanikio huwa tunabweteka na kufikiri kuwa tumefika.

Eneo hili huwa ni eneo baya sana eneo ambalo linalokufanya udhani umemaliza kila kitu 

Kwanini eneo hili ni baya?

Kwakua ukifika kwenye eneo hilo huwatunaacha kufanya vitu vile vilivyotufanya tukafikia hapo na kwakua tunaacha kufanya vitu hivyo muda si mrefu tutashuka , na kufilisika kabisa.

Ili tuwe na mafanikio tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii (worked hard) , kujisukuma kwa lazima (pushed), 

Kwa hakika tunapoacha kufanya hayo kwa kuanza kujiambia kuwa "hata hivyo tumefanya mno ,tukae tupumzike eti" 
Nikwambie Rafiki maneno hayo yanachochea ushukaji wa kiwango cha juu na kukufanya udidimie Mara dufu.

Kwa mfano wakati tulipokuwa tunataka kufanikiwa tulifanya haya:-

a). Tulikuwa wasikilizaji wazuri.
b). Tulikuwa wachambuzi wazuri
c). Tulikuwa watatuzi wazuri wa matatizo
d). Tulikuwa waulizaji wazuri wa maswali
f). Tulikuwa wavumilivu wazuri sana.
g).Tulikuwa watengenezaji wa mitandao mizuri ya watu waliotupatia mawazo bora yaliyotupatia mafanikio.

Lakini Leo yote haya tumeyaacha eti kwasababu tumegundua tulifanya mno kazi na sasa tunajiambia "fedha itajileta yenyewe, mawazo yatakuja yenyewe tu,
Nakwambia tunajidanya katika kuyafikia mafanikio tujikite zaidi kwenye kufanya zaidi si kama mwanzo tutafurahia mafanikio yadumuyo.

Uwe na siku njema kumbuka mafanikio ni safari isiyo kuwa na Mwisho.


No comments:

Post a Comment