Nchini kwetu na duniani kwa ujumla kunashuhudiwa ukosefu na uhaba wa ajira haswaa kwa vijana waliomaliza elimu zao , ambao wapo tayari kuajiriwa. Ni jambo la kusikitisha sana unaposikia nafasi za kazi zilizotangazwa ni tatu (3) kisha wanajitokeza waomba nafasi hiyo mamia ya vijana kwa nafasi tatu , ukiona hivi mwandishi wa kitabu cha the art of thinking in system Ndugu Steven Schuster anasema hayo ni matokeo ya watu kuwa na ufinyu wa fikra ama kushindwa kufikiri kwa kutumia mfumo wa kufikiri , Sitaki kukubalina naye ama kubishana naye kuwa na sisi hapa nchini kwetu huenda tupo hivyo lakini ukisoma mistari ndani ya kitabu kwa kina anasema pia janga hili la watu kushindwa kufikiri kimfumo ama kwa usahihi linawakumbuka asilimia 95%ya wakazi wa dunia hiii.
Kwa maana hiyo tunao wajibu wa kuja na majibu sahihi juu ya changamoto zinazotukabili na kama tutakosa majibu sahihi ni ukweli usiopingika kuwa hatufikiri vizuri na kizazi chetu kitakuja kutulaani kwa kuwa na wazazi wenye fikra finyu.
NINI KIFANYIKE KUKABILIANA NA UGUMU WA AJIRA NCHINI KWETU?
Kujibu swali hili nyeti na muhimu sana kwa jamii yetu , kwanza nieleze dhana mbili muhimu sana ambazo zinashauriwa kuchukuliwa kwa uzito kwenye nyanja ya kufikiri vizuri na kuja na majibu ya matatizo makubwa na magumu ambazo hutoa majibu ya kudumu kwa matatizo mazito na magumu.
1.Kufikiri kwa ubunifu (Lateral thinking).
Huu ni mfumo wa kufikiri kwa kutumia ubunifu kukabilina na jambo unalotaka kulipatia majibu , mfumo huu unamtaka anayefikiri kwenda hatua kwa hatua mpaka atakapo kuja na majibu sahihi juu ya tatizo husika , mfumo huu unayakubali mawazo yote na hutokeza njia za utatuzi ambazo hazina ukomo kwa hivyo mavumbuzi yanayofikiwa hayawi na majibu ya moja kwa moja.
2.kufikiri kwa kina (critical thinking).
Huu ni mfumo wa kufikiri kwa kuhusisha hoja na pumba juu ya njia inayofikiwa kwenda kutatua tatizo na mwisho kuja na majibu sahihi.
Baada ya kueleza dhana hizo mbili sasa ni muhimu tuone kwa kufikiri kwa kutumia njia zote hizo mbili kupata majibu ya ukosefu wa ajira nchini kwetu na kama inawezakana kupitia njia hizo kuja na majibu ya kudumu kuondokana na tatizo hili rahisi kwenye jamii yetu.
MAWAZO MBADALA.
1.Kuanzishwe umoja wa wasio na ajira.
Umoja huu utakuwa na kazi kuu mbili muhimu, kwanza itakuwa ni kutambuana na pili kutafutiana/kubuni ajira kwa ajili ya wanaumoja.
2.Uwepo wa ajira za kipindi kifupi mpaka cha kati (miezi 6- miaka 10).
Ajira zote nchini ambazo zinatoka kwa kudumu mpaka mwajiriwa astaafu ama kutasfishwa kwa lazima zibadilishwe na zianze kutolewa kwa kipindi kifupi na cha kati ili kuwapa wengine upenyo wa kuajiriwa na kujipatia ridhiki na wakati mwingine mitaji ya kudumu kuanzishia miradi endelevu.
Faida nyingine kutokana na kuanzisha hilo tutakuwa na uwezo wa kuboresha utendaji kazi kwa watumishi na kuinua viwango vya uzalishaji kwenye sekta mbalimbali kwa mfano kwenye elimu mwalimu atakayefanya vizuri kwa kujituma kufundisha na kuleta ubunifu kwenye kazi yake ajira yake italindwa na ataongezewa muda mwingine na yule aliyefanya hovyo ataondolewa na kuajiriwa mwingine.
3.Serikali ianzishe vijiji vipya na maalumu kwa wasomi wasio na ajira.
Mpango huu uende sambamba na kuyabaini maeneo yanayoweza kuendeshea shughuli za kilimo kwa muda wote kwa mwaka vijana wa kiume na wakike wawekwe kwenye vijiji hivyo kwa maana ya kuanza maisha ya msingi kujenga jamii yao mpya kwa kufanya magunduzi na ubunifu kutoka kijijini hapo kwa mfano kuanzisha kilimo cha kufa na kupona na serikali iwe tayari kutoa vifaa saidizi vyote kwa kuanzia miezi sita ya mwanzo na wakiivisha mazao serikali iwe tayari kuwatafutia masoko ama kununua bidhaa hizo zitakozo kwenye vijiji vya wasomi wasio na ajira.
4.Nafasi za kisiasa zipunguziwe mishahara /kuwepo ukomo wa muda kugombea wagombea walewale.
Kila mmoja anafahamu kuwa nafasi za kimadaraka nazo hutumika kama njia mbabadala kwa ukosefu wa ajira maana nazo zina ujira , kuliona hilo kunaweza kufanyika namna bora kwenye eneo hilo napo tukawapata wengi wakinufaika na keki hiyo.
unaruhusiwa kusasahihisha ,kurekebisha na pia kuongeza njia mbadala....
NDIMI MICHAEL THE GREAT ONE MWANAGENZI
No comments:
Post a Comment